Wanafunzi wa Chuo cha Kidini cha Wasichana cha Hazrat Zainab (as), Kigamboni, Dar es Salaam, Tanzania, pamoja na wasimamizi wao, wamehudhuria katika Majlisi ya maombolezo ya kumbukumbu ya Shahada ya Imam Hassan (as), iliyoanza kwa usomaji wa Qur’an Tukufu na kufuatiwa na muhadhara kuhusiana Fadhila za Imam Hassan (sa) na tukio zima la Shahada yake.

22 Julai 2026 - 22:34

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Chuo cha Dini cha Wasichana cha Hazrat Zainab (as) kilichopo Kigamboni, Dar es Salaam, Tanzania, kimeendesha Majlisi maalum ya Maombolezo kwa ajili ya kuadhimisha kumbukumbu ya Shahada ya Imam Hassan al-Mujtaba (as).

Wanafunzi wa Hawzah ya Hazrat Zainab (sa) Wakuhuisha Majlis ya Maombolezo ya Shahada ya Imam Hasan (as) Nchini Tanzania +Picha


 Majlisi hiyo imefanyika leo hii Jumatano, tarehe 22 Julai 2026, ikihudhuriwa na jumla ya wanafunzi 144, pamoja na wasimamizi wao.
 
Katika Majlisi hiyo, Qur’an Tukufu ilisomwa na mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho, ikiwa ni sehemu ya programu ya kiroho na kidini ya kuwaenzi Maimam watukufu wa Ahlul-Bayt (as).
 
Aidha, mihadhara mbalimbali ya Kidini ilitolewa na wapenzi wa Ahlul-Bayt (as), ambao ni Wanafunzi wa Hawzah hiyo na ambao walieleza mambo mbalimbali yanayohusiana na maisha, mafundisho na msimamo wa Imam Hassan (as).
 
Majlisi hiyo iliandaliwa na Chuo cha Dini cha Wasichana cha Hazrat Zainab (as), Kigamboni, Tanzania, ikiwa ni sehemu ya kuendeleza utamaduni wa kuwakumbuka na kujifunza kutoka kwa viongozi wa Ahlul-Bayt (as).
 

Maoni yako

You are replying to: .
captcha